Macho na masikio ya maelfu ya watu duniani yanasubiri kuona itakavyokuwa harusi ya mtoto wa mfalme wa Wales Uingereza Prince Harry na mchumba wake Meghan Markle itayofanyika May 19, mwaka huu.
Ikulu ya Mfalme Uingereza inaendelea kutoa taarifa kidogo kidogo za jinsi ambavyo harusi hiyo itakuwa ikiwa ni pamoja na kuweka wazi harusi hiyo itahudhuriwa na wageni zaidi ya 600.
Inaelezwa kuwa baadhi ya vipande vya keki ya harusi vya wawili hawa vitauzwa kwenye mnada, pamoja na keki za maharusi waliopita wa familia hiyo ambao ni Prince Charles Princess Diana (wazazi wa Prince Harry) na Prince William na Kate Middleton (Kaka wa Prince Harry na mkewe).
Vipande hivyo ambavyo vitakuwa vitano vitapigwa mnada kwa maelfu ya Dola za Kimarekani. Hatahivyo inaelezwa kuwa keki hizo sio za kuliwa.
MWISHO WA YOTE: Watanzania kuanza kupima UKIMWI kwa mate?