Mkurugenzi wa Utetezi wa Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Anna Henga amesema ili sheria iwe nzuri lazima watumiaji waielewe.
Henga ameyasema hayo kwenye mkutano wa wadau wa habari, vijana, na asasi za kiraia waliokutana kujadili kanuni mpya za mitandaoni.
Amesema kuwa muda uliotolewa na mamlaka husika kutoa maoni yao kuhusu kanuni hizo ulikuwa ni mdogo, hivyo kusababisha watumiaji wengi kutokuwa na uelewa juu ya suala hilo.
“Sheria ili iwe nzuri lazima watumiaji waielewe, ndio maana tumekutana hapa kujadili kanuni hizo ambazo zimepitishwa bila kusikilizwa kwa maoni ya watumiaji,”.
Pia Henga amesema kuna baadhi ya vipengele vya kanuni hizo ni vizuri lakini vingine ni vibaya kwa kuwa vinaminya Uhuru wa habari na kujieleza.
JAJI MKUU – “Tunataka hukumu kuanza kutolewa kimtandao’ –