Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hellen Mwingira kwa kosa la kujifanya Afisa wa TAKUKURU, huku akifanya udanganyifu na utapeli katika maofisi.
Mshtakiwa huyo amesomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 4 ya mwaka 2018, mbele ya Hakimu, Wilberforce Luhwago.
Wakili wa TAKUKURU, Veronika Chimwanda amedai kuwa mshtakiwa Mwingira kwa nyakati tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam alijifanya Ofisa wa Takukuru wakati alipokwenda kujitambulisha Wizara ya Kazi na Ajira na kufanya udanganyifu na utapeli katika kampuni ya mabasi ya Said Baba.
Baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka hilo alikana na upande wa mashtaka amedai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi May 8, 2018 kwa ajili ya kutajwa, ambapo mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaominika ambapo kila mmoja atasaini bondi ya Sh.Mil 3.
Hata hivyo mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti hayo, hivyo amepelekwa rumande.
VURUGU: Abiria wa mwendokasi walivyogoma leo KIMARA