Leo May 8, 2018 moja stori ambayo inashika headlines mtandaoni ni hii ya Tanzania kuorodheshwa kuwa miongoni mwa nchi ambayo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi kufikia mwaka 2026.
Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo cha Chuo Kikuu cha Havard cha Marekani kinakadiria kwamba, uchumi wa Tanzania utakuwa kwa asilimia 6.15 wakati huo.
Tanzania itakuwa nchi ya nne kwa uchumi wake kukua kwa kasi zaidi kufikia 2026.
India ndiyo itakayoongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi ya 7.89 ikifuatiwa na Uganda (7.46) na Misri ya tatu (6.63).
Ripoti hiyo ya Havard ilibaini kwamba kampuni ambazo zimefanya mabadiliko chanya na kuingiza uchangamano katika sekta mbalimbali za uchumi kwa mfano India na Vietnam ndizo zitakazokua kwa kasi zaidi katika muongo mmoja ujao.
Baada ya Uganda na Tanzania, Kenya ni ya kumi katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kukua kwa kasi zaidi mwaka 2026 ambapo ukuaji wake utakuwa asilimia 5.87.