Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wakimbizi UNHCR nchini Uganda, Joel Boutroue ameeleza kuwa huenda shughuli za shirika hilo kwa wakimbizi nchini humo zikakwama.
Ameeleza kuwa hii ni kutokana na ukosefu wa fedha kutoka kwenye jumuiya za kimataifa kuendesha shughuli zao za kuhudumia mamilioni ya wakimbizi hao.
Boutroue ameeleza kuwa hadi sasa shirika hilo limepata asilimia 9 tu ya jumla ya fedha zote walizoomba katika bajeti yao ya Dola Milioni 450 sawa Shilingi za Kitanzania Trilioni 1.08 kwaajili ya matumizi ya mwaka huu.
Hadi kufikia mwezi August 2017, Uganda ilikuwa inahudumia wakimbizi milioni 1.3, idadi ambayo UNHCR wanasema watashindwa kuihudumia ipasavyo.
UDART kuhusu tatizo la usafiri, Je wana mpango wa kuhama Jangwani?