Mpango wa Umoja wa Mataifa kuondoa kituo chake cha kikanda kilichopo jijini Entebbe na kukihamishia Nairobi Kenya kimepingwa vikali na serikali ya nchi hiyo.
Inaelezwa kuwa Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres na kumweleza kutoridhia pendekezo hilo la kuondolewa kwa kituo hicho.
Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Kadaga ameteuwa Kamati ya Bunge ya masuala ya mambo ya nchi za nje pamoja na Mbunge Theodore Sssekikubo kulifuatilia suala hilo.
“Tunaomba huu mchakato ufanyike haraka”- Ngeleja