Usiku wa May 6 2018 mchezo wa kwanza wa Yanga wa Kundi D wa Kombe la shirikisho Afrika ulichezwa mjini Algers nchini Algeria dhidi ya wenyeji wao USM Alger, game hiyo Yanga walipoteza kwa magoli 4-0, baada ya kipigo hicho utani umekuwa ukiendelea kwa Yanga kupoteza mchezo huo.
Imekuwa ni kawaida kwa wabunge kuwa na utamaduni wa kupenda kutaniana pale ambapo timu moja wako kati ya Simba au Yanga inapoteza basi wabunge wanaoshabiki moja kati ya timu ambayo imeshinda wanashangilia au wanatania mashabiki wenzao wa timu iliyofungwa.
Mwenyekiti wa matawi ya Yanga SC Bakili Makele leo ameongea na vyomba vya habari na kueleza kusikitishwa kwake kwa baadhi ya wabunge kuleta utani baada ya Yanga kufungwa magoli 4-0, hivyo anaamini hawakupaswa kufanya hivyo kwa sababu Yanga ilikuwa inawakilisa nchi.
VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL