Usiku wa May 9 2018 Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 imeendelea wa kwa michezo minne kuchezwa, timu nyingi zimebakisha game moja moja Ligi Kumalizika lakini vita ipo ni timu gani zitashuka daraja na timu gani zitapata nafasi ya kucheza Champions League.
Club ya Tottenham Hotspurs baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Newcastle United sasa ni rasmi wanakuwa wamekata tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Champions Leagu msimu wa 2018/2019 na vita ya nafasi ya moja iliyosalia wameiachia kwa Chelsea na Liverpool.
Ushindi wa Tottenham wa leo umewafanya wavune jumla ya point 74 point ambazo kwa Chelsea hawezi kuzifikia ni Liverpool pekee hivyo hata kama Chelsea akishinda game yake ya mwisho dhidi ya Newcastle na Liverpool akapoteza dhidi ya Brighton, bado hawezi kuzifikia point za Spurs.
Kufuzu au kupata tiketi kwa Chelsea ya kushiriki michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 kunategemeana na Liverpool hadi apoteze mchezo dhidi ya Brighton wakati wao Chelsea wakiwa ugenini watalazimika kuhakikisha wanapata ushindi ili wamalize nafasi ya nne katika msimamo wa msimu wa 2017/2018.
VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL