Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa ndani wa kesi inayomkabili mmiliki wa IPTL, Harbinder Sethi na mwenzake umekamilika isipokuwa kinachowasumbua ni upelelezi kutoka nje ya nchi.
Hayo yameelezwa na Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo amedai kuwa upelelezi wa ndani wa kesi hiyo umekamilika na umepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Swai amedai kuwa licha ya kukamilika kwa upelelezi wa ndani, bado wanasumbuliwa na upelelezi uliopo nje ya nchi.
Pia Swai ameeleza kuwa wametekeleza amri ya mahakama kwamba Sethi apelekwe Hospitali ambapo amepewa majibu ya vipimo alivyofanyiwa na ameambiwa kuna daktari yupo nchini Misri akirudi watakamilisha matibabu yake.
Wakili wa Sethi, Dora Mallaba alilalamika kuhusu mke wa Sethi kuzuiwa kuonana na mumewe pale anapokwenda gerezani kumuona.
Wakili Dora alidai kuwa kibali cha mke wa Sethi kumuona mumewe gerezani kiliombwa tangu mwezi February hadi Leo hakijatoka hivyo aliiomba mahakama itoe maelekezo ili mkewe aweze kumuona.
Baada ya kusikilizwa hoja hizo, Hakimu Shaidi amesema kuhusu kuonana na mtu aliyekuwepo magereza ni suala la magereza ila kibinadamu hao ni mtu na mkewe na wanapendana hivyo alishauri wapewe nafasi ya kuonana.
Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi May 25,2018 Kwa ajili ya kutajwa.
Watu wa Mbeya walivyompokea Sugu katika ofisi ya CHADEMA