Baada ya kiungo wa Man City Yaya Toure kuagwa rasmi na wachezaji na viongozi wa timu ya Man City baada ya kudumu katika club hiyo kwa miaka nane toka alipojiunga nayo mwaka 2010 akitokea club ya FC Barcelona ya Hispania, wakala wake Dimitri Seluk ameongea na kuweka wazi anachokiamini.
“Yaya alikuwa ni moja kati ya wachezaji wa mwanzoni kusainiwa na Man City wakati Sheikh Mansour alipoamua kuifanya Man City kuwa club kubwa na Yaya amefanya vizuri Man City lakini leo sio ndio mwisho wa kucheza soka kwa Yaya Toure bado ataendelea kucheza England na atadhihirisha kuwa anaweza kucheza kwa kiwango kikubwa”>>>Dimitri
“Labda siku moja Yaya atarudi ManCity kama mchezaji, kocha, mkurugenzi wa michezo tutaona, Yaya moyo wake upo Manchester City labda baada ya mwaka mmoja au miaka miwili Guardiola ataondoka Man City na Yaya atarudi maana hakuna anayejua, Yaya atathibitisha ubora wake inawezekana hakuwa anafiti katika mfumo wa Guardiola lakini tutamuona msimu ujao”>>> Dimitri
Kwa mujibu wa maelezo ya wakala wa Yaya Toure kuna uwezekano au dalili kubwa za Yaya Toure mwenye umri wa miaka 34 akacheza msimu ujao katika Ligi Kuu England akiwa na club nyingine tofauti, Toure msimu huu amepata nafasi ya kuichezea Man City katika mechi 16 pekee na kati ya hizo nne za Carabao Cup.
VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL