Alhamisi ya May 10 2018 ni moja kati ya siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenda soka la Bongo hususani mashabiki wa club ya Simba ambao wanautolea macho mchezo kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga katika uwanja wa Sokoine Mbeya.
Mvuto wa mchezo wa Prisons dhidi ya Yanga kuwa na mvuto kwa mashabiki wa Simba kunatokana na kuwa game hiyo kama Yanga akitoa sare au kupoteza basi Simba atakuwa Bingwa wa VPL moja kwa moja akiwa amesalia na michezo mitatu mkononi.
Game ya leo Tanzania Prisons imeivua Ubingwa Yanga kwa kuifunga magoli 2-0, magoli ya Prisons yakifungwa na Eliuter Mpepo kwa mkwaju wa penati dakika ya 58 na Salum Bosco dakika ya 85, Yanga amesaliwa na michezi mitano na ana point 48 hivyo hata akishinda game zote hawezi kufikia point 65 za Simba kwani atakuwa na point 63.
Simba baada ya kiu ya muda mrefu hatimae wanatwaa taji lao la kwanza la VPL baada ya miaka sita, mara ya mwisho Simba kutwaa Ubingwa ilikuwa ni msimu wa 2011/2012 toka hapo Simba hajawahi kutwaa Ubingwa wa VPL, hivyo Simba leo wanatwaa taji hilo wakiwa wanaangalia game kwenye TV kama ilivyokuwa kwa Man City walivyotwaa Ubingwa wa EPL msimu wa 2017/2018.
VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL