Binti wa miaka 19 kutoka nchini Sudan, amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumchoma kisu hadi kifo mumewe kwa madai kwamba alimbaka.
Binti huyo anayefahamika kama Noura Hussein anadaiwa kulazimishwa kuolewa na mwanaume huyo na alipokataa kufanya naye mapenzi, mwanaume huyo alimbaka, wakati binti huyo akiwa ameshikiliwa na ndugu wa mumewe huyo.
Kesi hii imeibua hisia nyingi nchini Sudan, wengine wakiafiki adhabu hiyo ya mahakama dhidi ya binti huyo huku wengine wakieleza kuwa kesi hii iwe mwanzo wa sheria ya ndoa za utotoni kubadilishwa.
Nchini Sudan, umri unaokubalika kisheria kuoa na kuolewa ni miaka 10 huku kubakwa na mume ni halali kisheria.
Msaada alioupata Mlemavu aliyekimbiwa na Mume na kuachiwa Mtoto