Mbwana Samatta May 10 2018 ameichezea KRC Genk kwa dakika 36 akitokea benchi dakika ya 54 kuchukua nafasi ya mgiriki Nikolaos Karelis timu yao ikiwa nyuma kwa goli 1-0 wakati huo, dakika 12 baada ya Samatta kuingia akafanikiwa kuisawazishi KRC Genk goli na kuufanya mchezo kumalizika kwa kufungana goli 1-1.
Samatta alipoulizwa kuhusu kufunga goli lake la kwanza baada ya kutoka majeruhi na kucheza dakika 1015 “Kilikuwa ni kipindi kigumu kuwa katika hali hiyo, mimi ni mshambuliaji nilikuwa majeruhi na sasa nimerudi japo ilikuwa ni ngumu kurudisha kiwango changu”
“Hivyo nikajitahidi na kuwa mvumilivu na nikasema utafika wakati wa kufunga na leo nimefunga najihisi kama nimetoka jela na hali yangu ya kujiamini imerudi na imani nitafunga tena kabla ya kumalizika kwa msimu” –@samagoal77
Mara ya mwisho Mbwana Samatta kuifungia goli KRC Genk kabla ya game ya May 10 2018 ikuwa October 25 2017 katika mchezo dhidi ya Club Brugge, ambapo Genk walipata ushindi wa magoli 2-0, ambapo Samatta alifunga goli la pili dakika ya 90.
Simba kama Man City tu wametwaa Ubingwa wa Ligi nje ya uwanja leo