Leo May 14, 2018 Kesi ya mauaji inayowakabili watu wanne akiwemo Afisa Mwandamizi wa Kanisa la International Evangalism Church (IEC), Obadiah Nanyaro(60) imeahirishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha baada upelelezi kutokamilika.
Kesi hiyo inawakabili watu hao ambao wanatuhumiwa kumuua aliyekuwa Mchungaji wa kanisa la Africa Mission Interantional marehemu, Nixon Issangya.
Mbele ya mahakama ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Nestory Baro mwendesha mashtaka wa serikali, Rose Sulle alieleza kuwa upelelezi juu ya kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba kuahirishwa hadi tarehe nyingine.
Mara baada ya ombi hilo ndipo hakimu Baro aliahirisha kesi hiyo hadi May 28 mwaka huu ambapo itakuja kwa ajili ya kutajwa.
Katika kesi hiyo watuhumiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na kosa la mauaji katika nambari 18 ya mwaka 2018.
Wanaokabiliwana kosa hilo ni Ndewario Issangya(59) mkazi wa Sakila chini Kikatiti, Simon Kaaya(42) mkazi wa Sakila Chini Kikatiti sanjari na Joshua Pallangyo(42) mkazi wa Sakila Chini Kikatiti.
Watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa mnamo April 7 mwaka 2017 katika eneo la Moivaro ndani ya jiji la Arusha washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa kwa kumuua Issangya ambaye alikuwa ni mkazi wa eneo la Sakila Chini Kikatiti.
Katika kesi hiyo watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo la mauaji kinyume na kifungu cha 196 cha sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.
LIVE MAGAZETI: Zengwe laibuka CCM, Polisi atekwa na wasiojulikana