Utafiti uliofanywa hivi karibuni na chuo kikuu cha utafiti wa afya wa magonjwa ya akili cha Ludwig-Maximilian mjini Munich ambao ulikagua tofauti za kiafya kati ya watu wanaochelewa kuamka na wanaowahi kuamka, ulionyesha hali sio nzuri sana kwa wanaochelewa kuamka
Hatari ya kifo cha mapema, matatizo ya akili na magonjwa yanayotokana na kupumua ndio mambo yaliyogunduliwa katika utafiti huo.
Utafiti huo uliunga mkono kulala mapema na kuamka mapema ili kuimarisha afya.
Utafiti huo pia umesema kuwa watu wanaoamka mapema na kufanya kazi ambazo huwalazimu kuchelewa kulala nao pia watakabiliwa na matatizo ya afya.