Usiku wa May 16 2018 fainali ya michuano ya UEFA Europa League msimu wa 2017/2018 ilichezwa mjini Lyon nchini Ufaransa kwa kuzikutanisha club za Atletico Madrid ya Hispania dhidi ya Olympique Marseille ya Ufaransa mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.
Marseille licha ya kuwa katika ardhi ya nchi yao lakini wameshindwa kulibakiza Kombe hilo nchini Ufaransa kwa kujikuta wakikubali kipigo cha magoli 3-0, magoli ya Atletico yakifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 21 na 49 wakati goli la mwisho likifungwa na Gabriel Fernandez dakika ya 89.
Ubingwa huo sasa ni heshima pia kwa Fernando Torres ambaye ametangaza kuwa huu ndio msimu wake wa mwisho kuichezea Atletico Madrid lakini kama hufahamu tu taji hilo linakuwa ni taji la pili la Europa League kwa Atletico Madrid chini ya kocha Diego Simeone ambaye pia ameiongoza timu hiyo kufika hatua ya fainali ya Champions League na kutwaa mataji ya Copa del Rey, Super Copa, Super Cup na LaLiga.
Haji Manara alivyokuja na takwimu leo mbele ya waandishi wa habari