Mbunge wa Monduli Julis Laizer alisimama Bungeni Dodoma kuchangia mapendekezo yake katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na uvuvi kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambapo ameilaumu Serikali kwa kitendo cha kukusanya kodi kwa wafugaji na wavuvi lakini imeshindwa kutenga fungu kwa ajili ya kuwaboreshea mazingira yao ya kazi.
“Serikali inatafuta ugomvi kwa wakulima na wafugaji, miaka mitatu mfululizo mnakusanya kodi lakini hampeleki huduma. Waziri unakubalije kumeza dhambi hii? Unakusanya kodi billion 26 alafu kwenye bajeti yako hujapeleka hata shilingi. Huu ni unyang’anyi mtuambie tumewakosea nini sisi wafugaji na wavuvi”- Julis Laizer
Mbunge aliyemwaga machozi Bungeni “wamekufa Wabunge mashahidi”