Sakata la kusaini mkataba mpya kwa mshambuliaji Wayne Rooney katika klabu ya Manchester United linaweza kufikia mwisho wiki baada ya mshambuliaji huyo kukubaliana na dili jipya alilopewa na mabingwa wa England.
Rooney na maofisa wa United walikuwa kwenye mazungumzo juu ya dili la mkataba mpya wa miaka minne ambao utamfanya muingereza huyo kuvuna kiasi cha £300,000 kwa wiki, na kufanya ndoto ya klabu ya Chelsea kumsajili iendelee kuwa ndoto.
Mkataba huo umeshindikana kutiwa saini kwa sababu Rooney na kocha David Moyes wapo Dubai na timu nzima kwenye mazoezi.
Hata hivyo, mtandao wa Dailymail unaripoti kwamba tangazo la dili jipya la Rooney litatolewa kabla ya United haijakutana na Crystal Palace katika Barclays Premier League wikiendi ijayo..