Bado siku tuweze kushuhudia fainali za Kombe la dunia 2018 zitakazochezwa nchini Urusi kwa kukutanisha mataifa 32, kukipiga kuwania Kombe hilo, najua umesikia majina ya baadhi ya mastaa wakiachwa na timu zao mwaka huu kama Cesc Fabregas na Alvaro Morata walioachwa na Hispania.
Leo kikosi kamili cha wachezaji 23 wa watakaoiwakilisha Ubelgiji katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 kimetajwa na kukosekana kwa jina la kiungo wa club ya AS Roma Radja Nainggolan ambaye alikuwa anatarajia kuwa sehemu ya kikosi hiko.
Radja Nainggolan baada ya kutangazwa kuwa hatokuwa sehemu ya kikosi cha Ubelgiji katika fainali hizo za Kombe la Dunia, ameamua kutangaza maamuzi ya kustaafu jumla kuichezea timu ya taifa ya Ubelgiji na kueleza kuwa atabaki kuwa shabiki tu.
“Soka langu la kimataifa kwa sasa limefikia mwisho, nimefanya kila kitu ili niwe sehemu ya kikosi na kuiwakilisha nchi yangu, kwa bahati mbaya sikuchaguliwa kuwa sehemu ya kikosi, kuanzia siku ya leo na kuendelea nitabaki kuwa shabiki namba moja wa Ubelgiji”>>> Radja Nainggolan
Nikukumbushe tu Radja Nainggolan akiwa na AS Roma msimu huu katika michuano ya UEFA Champions League na Ligi Kuu Italia Serie A anakuwa miongni mwa wachezaji wachache waliyotengeza 11 na kuendelea, namba mbili kwa kutengeneza nafasi 79 na namba nne kwa wachezaji waliyowin tacles nyingi 67.
VIDEO: Wachezaji wa Simba SC baada ya kukabidhiwa Kombe la VPL