Leo May 22, 2018 kuna hii ya kuifahamu ni Mahakama moja nchini Uturuki imewahukumu kifungo cha maisha watu 104 kwa kuhusika katika mapinduzi yaliyoshindwa ya mwaka 2016.
Watu 104 kati ya 280 wamepewa kifungo cha maisha jela, kifungo ambacho ni adhabu ya juu zaidi kwa mujibu wa katiba ya Uturuki.
Washukiwa wengine 21 walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kumtusi rais, huku wengine 31 wakihukumiwa miaka 10 na miezi sita kwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi.
Watu 240, waliuawa usiku wa July 15, 2016, pale kundi la wanajeshi waasi waliamuru vifaru kuelekea barabarani pamoja na ndege za kivita katika jitihada zao za kumpindua Rais Tayyip Erdogan.