Bado siku 23 fainali za Kombe la Dunia 2018 zianze kutimua vumbi nchini Urusi kwa mataifa 32 kuchuana, maswali yamekuwa mengi kwa baadhi ya mashabiki wa soka kufuatia maamuzi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez kumuacha kiungo wa AS Roma Radja Nainggolan.
Martinez ameeleza kuwa ilikuwa ni wakati mugmua kuamua kumuacha kiungo mkongwe wa Ubelgiji Radja Nainggolan kutokana na Ubelgiji kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo mzuri lakini sababu za kumuacha Nainggolan amezitaja kuwa ni sababu za kimfumo.
“Sababu za kumuacha Radja ziko wazi kabisa ni sababu za kiufundi, katika miaka miwili iliyopita timu ilikuwa ikicheza katika mfumo wa kushambulia na wachezaji wengine walikuwa na kazi yao, ukimzungumzia Radja ni kweli amefanya vizuri akiwa na club lakini sidhani kama naweza kumtumia timu ya taifa”>>> Roberto Martinez
Kocha mkuu wa Ubelgiji Roberto Martinez ameeleza kuwa mfumo wake ndio umemfanya amuache kiungo mkongwe Radja Nainggolan Kombe la dunia na alienda Roma Italia kufanya nae mazungumzo #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/gkz5erWQAl
— millardayo (@millardayo_) May 22, 2018
VIDEO: Wachezaji wa Simba SC baada ya kukabidhiwa Kombe la VPL