Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) António Guterres amemteua Joyce Msuya ambaye ni Mtanzania kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Program ya Mazingira ya UN. Program ya Mazingira ofisi zake zipo nchini Kenya.
Kabla ya kuteuliwa Joyce Msuya alikuwa Mshauri wa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Asia ya Mashariki na maeneo ya Pacific huko Washington DC.
Joyce Msuya anachukua nafasi ya Ibrahim Thiaw wa Mauritania ambaye alitumikia nafasi hiyo tangu mwaka 2013.