Leo May 22, 2018 Chama cha Wafanyakazi (TAMICO) kimesema baadhi ya Watanzania wanakuwa kama Watumwa katika ardhi yao kutokana na kusainishwa mikataba mibovu na ya kulazimishwa katika maeneo ya kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa wa TAMICO, Jonas John amesema mathalani wamekuwa na mgogoro na kampuni ya Ujenzi ya CRJE kuhusu suala la kusitisha na kulazimisha mikataba ya wafanyakazi kinyume na sheria.
John amesema kuwa licha ya migogoro waliyonayo, hivi karibuni kampuni hiyo imewazuia zaidi ya wafanyakazi 40 baada ya kugoma kusaini mikataba ambayo inaminya haki zao na haiwapi fursa ya kuiisoma.
“Ni wakati wa serikali ijue kuwa kuna Watanzania wanakuwa watumwa katika ardhi hii kutokana na kunyimwa stahiki zao katika maeneo ya kazi,”
Amesema kuwa wamekuwa katika majadiliano jinsi ya kuhamisha wafanyakazi na kusainishwa mikataba mipya lakini wanashangazwa kuon wafanyakazi wanafungiwa nje.
Naye Hassan Seif amesema yeye ni mfanyakazi wa kampuni hiyo tangu ilipoanzishwa na ana miaka 40 sasa katika kampuni hiyo.
“Nimefanya kazi miaka 40 kisha wanataka kunilipa kiinua mgongo cha Laki 2, amekuja muwekezaji mpya wanaturadhimisha kusaini mikataba mpya kinyume na sheria,” amesema Seif.