Leo May 23, 2018 Moja ya stori ya kuifahamu ni kuhusu Watafiti kutoka Taasisi ya Novo Nordisk Research and Development ambapo wameonya kuwa kama aina ya mfumo wa maisha uliopo sasa utaendelea basi ifikapo mwaka 2045 asilimia 22 ambayo inakaribia robo ya watu wote duniani watakuwa na uzito uliopitiliza.
Aidha utafiti hiyo pia umeeleza kuwa asilimia 12 ya watu wote duniani watakuwa na maradhi ya kisukari daraja la pili ifikapo mwaka 2045.
Aidha katika ufanyaji wa tafiti hiyo, watafiti walifanya uchambuzi wa idadi ya watu wote duniani.