Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo May 24, 2018 amewataka Wizara ya Fedha kujitathmini au kueleza kinachokwamisha wao kushindwa kutoa malipo ya fedha za korosho kwa wananchi ambazo ni za kwao.
“Mtu analaumiwa wala sio mkosaji Wizara ya fedha kuna mambo yanaendelea huko sasa sisi tunakuwa hatujui tunawaona nyie wabaya, kwa nini ukae na hela mtu anakuomba, anakulambalamba na hela ni yake, ebu mjitathmini” amesema Spika Ndugai