Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeombwa kuangalia kwa undani zaidi kwa kuanzisha kitengo kitakacho angalia suala la ugonjwa hatari Systemic Lupus Erythematosus(SLE).
Ugonjwa huo ambao hadi sasa haujajulikana chanzo chake na kwamba hauna tiba huku dalili zake zikiwa si za kuthibitika.
May 3, 2018 Daktari Bingwa wa Usingizi kwa Watoto na Wagonjwa Mahututi pekee, wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Onesmo Mhehwa alifariki dunia kwa ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa na Balozi Chabaka Kilumanga, ambapo amesema mbali na kuanzisha kitengo hicho pia kuangalia namna ya kuwapata wataalamu ambapo wataushughulikia ungonjwa huo ambao ni hatari.
Alisema mke wake Irene Kilumanga anaishi na ugonjwa huo tangu mwaka 2007 hadi sasa ni miaka kumi.
Balozi Kilumanga aliongeza kuwa watu wanaougua ugonjwa huo unaweza kuona wanafanya makusudi kutokana na kuugua kwa muda fulani na muda mwingine kuoneka akiwa mzima.
“Dk. Mhehwa amekuwa chanzo cha watu wengi kuanza kuujua ugonjwa huu baada ya kufariki na ndipo nilipoona Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janab akiizungumzia nikaona nimtafute ili tyushirikiane kuutangaza,” Dk. Kilumanga
Aliongeza kuwa nchi zilizoendelea wanaujua ugonjwa huo wa SLE ambapo kuna siku maalumu ya kuadhimisha ambayo ni May 10 kila mwaka.
Balozi Kilumanga alisema serikali ianze kuandaa wataalamu watakao bobea kutibu ugonjwa huo tofauti na ilivyo sasa.
Pia aliishauri serikali kununua vifaa vya kupimia ugonjwa huo ili watu waweze kugundulika mapema tofauti na ilivyo sasa ambapo wanaenda kugundulika nje ya nchi.
Kwa upande wake mke wa Balozi Kilumanga, Irene Kilumanga alisema kuwa ugonjwa huo ulimuanza tangu mwaka 2007 hadi sasa anaishi nao na kwamba dalili zake zinafanana na za malaria za kuhisi homa homa.