Leo May 27, 2018 Watu zaidi ya 50 wameripotiwa kufariki na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya mtumbwi waliokuwa wakosafiria kuzama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ajali hiyo imetokea katika mto Tshuapa Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ajali hiyo imetokea Monkoto kuelekea Mbandaka eneo ambalo kunapatikana janga la virusi vya Ebola tangu May 8.
Watu 50 wameripotiwa kufariki katika jali hiyo. Taarifa kuhusu ajali hiyo imetolewa na Naibu gavana wa Tshuapa Richard Mboyo Iluka.
LIVE MAGAZETI: Kinana ang’atuka CCM, Wamebeba, CHADEMA yapata pigo