Leo May 28,2018 tunayo story ya kisheria kuhusu vijana waliofikisha miaka 18, huku wakiendelea kukaa nyumbani na kushindwa kufanya kazi.
Mwanasheria wa kujitegemea Leonard Manyama anasema ni kosa kisheria na kinyume na Katiba kwa kijana mwenye zaidi ya miaka 18 kukaa nyumbani kwa wazazi wake na kutofanya kazi.
Anasema kwa mujibu wa sheria wazazi wana uwezo wa kumshtaki kijana wao ambaye hataki kufanya kazi na Mahakama ikaamuru aondoke nyumbani.
“Wazazi watafungua kesi ya madai na mahakama inaweza kuamuru aondoke nyumbani, endapo akikaidi anaweza kufungulia kesi ya jinai kwa kuidharau mahakama na adhabu yake ni kifungo cha miezi 6 jela,” amesema Wakili Manyama.