Rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina Mahmoud Abbas ameruhusiwa kutoka hospitalini leo May 29, 2018 siku nane tangu alipolazwa akiwa na matatizo ya mapafu.
Abbas mwenye miaka 83, amepata matatizo ya kiafya mara kadhaa na alipelekwa hospitali May 20 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uchunguzi baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo katika sikio lake.
Akizungumza mara tu baada ya kutoka hospitali kiongozi huyo amesema anatoka akiwa na afya njema na atarejea kazini kuendelea na majukumu yake hivi leo.
Tangu muhula wake kukamilika, Abbas ameendelea kutawala bila kufanyika chaguzi katika maeneo ya Wapalestina.