Ndoto za klabu ya Manchester City kuwa na uwanja mkubwa zaidi zimeanza kutimia mara baada ya madiwani wa baraza la jiji la Manchester kupitisha mpango huo.
Klabu hiyo ya Uingereza sasa itaweza kuutanua uwanja wake wa Etihad ambao unaingiza watu 48,000 mpaka kufikia kuingiza watu 62,000.
Mradi huu utajumuisha ujenzi wa maeneo mawili yatakayokuwa na mashabiki elfu nane zaidi.
Ujenzi huo utaifanya uwanja huo wa Etihad kuwa wa pili kwa ukubwa nchini Uingereza baada ya uwanja wa Manchester United wa Old Trafford.
Madiwani wa baraza la jiji la Manchester, waliidhinisha mradi huo, ambao unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Manchester City ilihamia uwanja huo mwaka wa 2003.
Awali Uwanja huo ulikuwa na idadi ya kuchukua mashabiki elfu thelathini na nane, wakati ilipojengwa mwaka wa 2002, kwa matumizi ya michezo ya Jumuiya ya madola.