Moja kati ya majina yaliotawala katika mitandao ya kijamii ni pamoja na jina la kijana wa Mali aliyezamia nchini Ufaransa kama muhamiaji haramu Mamadou Gassama kwa kitendo chake cha ushujaa cha kumuokoa mtoto.
Mamadou akiwa Paris Ufaransa katika pitapita zake alikuta watu wamesimama nje ya jengo refu na kuangalia juu wakiona mtoto akininginia ghorofani hivyo, Mamadou pasipo kuombwa wala nini alianza jitihada kwa kukwea gorofa hilo na kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Baada ya kitendo hicho Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimualika kwake na kumpa cheti cha ushujaa na kumpa uraia wa Ufaransa na kazi katika kitengo cha zimamoto na uokoaji, leo ameoneshwa akiwa tayari amewasili katika kikosi cha zimamoto.
TAARIFA YA HABARI: Watu watatu walivyocharangwa na Kisu jumba la FISI