Baada ya kuifundisha club ya Real Madrid ya Hispania kwa mafanikio akiwa kama kocha mkuu wa club hiyo Zinedine Zidane leo ametangaza maamuzi yaliowashitua wengi kuhusiana na hatma yake ndani ya club hiyo.
Zidane ambaye amewahi kuichezea Real Madrid kwa miaka mitano (2001-2006) kama mchezaji leo ametangaza kujiuzulu, Zidane aliapata nafasi ya kuwa kocha wa Real Madrid katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2016 akitokea timu ya Real Madrid ya wachezaji wa akiba (Real Madrid Castilla).
Maamuzi ya Zidane kuondoka Real Madrid yanatajwa ni kutokana na kutaka kulinda rekodi yake na sio vinginevyo, Zidane amefanikiwa kuiongoza Real Madrid katika michezo 149, akishinda michezo 104, sare 29, akipoteza game 16, mataji 9 na kufunga magoli 393.
Zidane ndio anakuwa kocha wa pili katika historia ya Real Madrid kuwa na mafanikio baada ya Miguel Munoz, aliyetwaa jumla ya mataji 15 Zidane akitwaa mataji 9.
Samatta na Omar Colley wameenda Macca