Klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine, imetangaza rasmi kwamba itaendelea kulipa mshahara wa mchezaji mbrazili Maicon ambaye alipata ajali na kufariki majuma mawili yaliyopita.
Shakthar wamesema fedha hizo za mshahara wa Maicon zitakwenda kwa familia yake iliyokuwa ikimtegemea mchezaji huyo aliyefarikia akiwa na miaka 25. demon
Akijibu maswali katika kipindi cha maswali na majibu na wapenzi wa klabu, raisi wa Shakhtar CEO Sergie Palkin alisema:
Mkataba baina yetu na Maicon ulikuwa unaenda mpaka mwaka 2015. Kwa kawaida kisheria baada ya kutokea tukio la hivi karibuni mkataba ungekuwa umevunjika, lakini ana mtoto wa miaka saba msichana na wazazi ambao ni wazee.
Kwahiyo, klabu imeamua kuendelea kulipa mishahara ya mchezaji kwa muda wote wa mkataba uliobakia ili iweze kuisadia familia yake.