Leo June 1, 2018 Mahakama ya jijini Milan nchini Italy imewaamuru wazazi waliokuwa wamempa mtoto wao jina la ‘Blu’ kumtafutia jina jingine mtoto huyo kwa sababu haliendani na jinsia ya kike ya mtoto huyo.
Kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2000 ya nchini humo inasema kuwa ‘jina la mtoto ni lazima lieandane na jinsia yake’.
Hivyo mahakama hiyo imewaamuru wazazi hao kumbadilishia jina au mahakama ndio impatie jina mtoto huyo kwa sababu jina hilo ‘Blu’ sio zuri kwa mtoto wa kike.
Aidha imeripotiwa kuwa wazazi hao wanajiandaa kuipa changamoto mahakama kwamba jina hilo linaweza kumfaa mtoto wa kike wakitolea mfano mtoto wa mastaa wasanii Jay Z na Beyonce ambao mtoto wao anaitwa ‘Blue Ivy’.
Msimamo wa Dk.Bashiru CCM ‘Siwezi kufanya siasa majukwaani’