Wanawake wanaopenda kula mara kwa mara vyakula aina ya Burger, Pizza na Kuku wa kukaanga wanachelewa kushika ujauzito halikadhalika wanatumia muda mrefu kushika mimba, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Human Reproduction iliyotoka alhamisi ya wiki hii.
“Kwa upande mwingine wanawake wanaopenda kula vyakula bora ikiwemo matunda wanawahi kushika ujauzito kwani vyakula hivyo huboresha mfumo wa uzazi na husaidia kupunguza muda wa mwanamke kushika mimba” alisema Profesa Claire Robers kutoka chuo kikuu cha Adelaide cha chini Australia.
Jessica Grieger ambaye ni mmoja wa timu ya utafiti huo amewashauri wanawake wanaotaka kushika ujauzito kufuata lishe pendekezwa kwa ajili ya ushikaji wa ujauzito.
Msimamo wa Dk.Bashiru CCM ‘Siwezi kufanya siasa majukwaani’