Leo June 1, 2018 taarifa nyingine kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Manya umeanza leo tarehe 01 Juni, 2018.
Kabla ya uteuzi huo Prof. Manya alikuwa Kamishna wa Madini na alikuwa akikaimu nafasi ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua David Mulabwa kuwa Kamishna wa Madini.
Kabla ya uteuzi huo Mulabwa alikuwa Kamishna Msaidizi wa Uchimbaji Mdogo.
Mulabwa amechukua nafasi iliyoachwa na Prof. Manya ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.
Uteuzi wa Mulabwa unaanza leo.