Leo June 4, 2018 kuna hii ya kuifahamu kutoka kwa Mary Harrison mwenye miaka 47 mkazi wa jiji la Dallas nchini Marekani ambaye amemuua mume wake Dexter Harrison kwa kumpiga risasi baada ya kumpiga paka wa familia.
Mamlaka ya jeshi la polisi Dallas, wamesema kuwa Marry amekamatwa na kuswekwa rumande kwa kosa la kumuua mumewe mwenye miaka 49 kwa kumpiga risasi na kufia baadae hospitalini.
Aidha polisi waliongeza kuwa ili Marry apate dhamana inahitajika dola 100,000 ambayo ni sawa na zaidi ya Milioni 228 za kitanzania.
Katika maelezo aliyoyatoa Marry katika kituo cha polisi jijini Dallas jumapili ya Juni 3 amesema kuwa, mume wake amekuwa na tabia ya kumpiga sana paka wao wa familia na alimpiga risasi Dexter jumamosi ya June 2 walipokuwa wakizozana juu ya tabia hiyo mbaya ya mumewe ya kumpiga paka.
Majirani wanasema kuwa paka huyo wa familia kwa siku za hivi karibuni alitoweka nyumbani lakini baadae alirudi huku Marry akiwa tayari ameshaanza kutangaza kutoweka kwa paka huyo.