Leo June 5, 2018 Ng’ombe mmoja mjamzito kutoka nchi ya Bulgaria amehukumiwa kufa baada ya kuvuka mpaka wa nchi yake na kuelekea Serbia kinyume na sheria.
Ng’ombe huyo ambaye jina lake anaitwa Penka alifanikiwa kuvunja zizi lake lililopo katika kijiji cha Kopilovtsi nchini Bulgaria karibu kabisa na mpaka wa Serbia na kuingia kimakosa katika mipaka ya nchi hio.
Ikumbukwe kuwa nchi ya Serbia sio mwanachama wa Umoja wa Ulaya hivyo ili mnyama aweze kuruhusiwa kuingia katika nchi hiyo kutoka nchi wanachama Umoja wa Ulaya inabidi awe na vibali maalumu ili aruhusiwe tofauti na hapo sheria inasema kuwa adhabu yake ni kifo.
Mmiliki wa ng’ombe huyo Ivan Haralampiev pamoja na mtoto wake wamekuwa wakimtafuta ng’ombe huyo mpaka siku moja waliposikia anashikiliwa katika kijii cha Bosilegrad nchini Serbia.
Aidha duru za kuaminika zinasema kuwa mmiliki huyo alijitahidi kwenda kumkomboa Penka lakini alishindwa baada ya mamlaka ya nchi hiyo kusema kuwa inasimamia sheria, na kwa mujibu wa sheria ni kuwa Penka lazima auawe kwa kuingia nchini Serbia kinyume na sheria.