Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba leo June 5 2018 amefanya ziara katika Bohari kuu la Jeshi la Polisi ambapo ndipo kuna maghala ya kuhifadhia vitu vya thamani kama silaha, sare za jeshi la polisi na magari ya polisi, pia kutembelea Bandari katika Kikosi cha Polisi cha Bandari .
Waziri Mwigulu ameongea na uongozi wa Polisi na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo kutoa wiki mbili kukamilisha timu za kufanya kazi katika maswala ya kiuchunguzi ili kujua hatma ya matatizo ya kimkataba, bei na ubora yaliyofanyika katika ununuzi wa sare la jeshi la polisi na magari ambayo yana makosa kimkataba.