Majaji Wakuu wa nchi 51 kutoka barani Afrika na wageni mbalimbali zaidi ya 200 wanatarajiwa kufika June 11 2018 katika mkutano mkubwa wa Kimataifa utakaofanyika Arusha hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanyika mkutano huo lengo likiwa ni kujadili mambo ya jinsia na utoaji haki.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo June 7 2018 Jaji Kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Dkt. Eliezer Feleshi na Msajili Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Katarina Revocati wamesema wanatarajia kupata wageni zaidi ya 350 ambapo mkutano utafanyikia AICC mpango mkakati ukiwa ni ufikiwaji wa haki popote.