Leo June 11, 2018 Mkutano wa kihistoria wa viongozi wa mataifa hasimu kwa muda mrefu Marekani na Korea Kaskazini ambao awali uliahirishwa sasa unaashiria kufanyika nchini Singapore kesho Jumanne katika kisiwa cha Sentosa baada ya viongozi hao kuwasili nchini humo kwa nyakati tofauti.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ndiye aliyeanza kuwasili Singapore na kisha Rais wa Marekani, Donald Trump naye akafuatia.
Marekani na Korea Kaskazini ni mataifa yanayokinzana tangu vita vya Korea vya mwaka 1950 hadi mwaka 1953 na viongozi wa nchi hizo hawajawahi kukutana wala kuzungumza kwa njia ya simu na mkutano huu wa Trump na Kim unatarajiwa kumaliza uhasama wa mataifa hayo kuhusiana na silaha za nyuklia za Korea Kaskazini suala ambalo lingeweza kuwaingiza kwenye vita.