Watu wengi hasa wadau wa michezo wanakua wakiwaangalia sana wachezaji waliotoka Bongo kwenda nje ya nchi kucheza soka la kulipwa na miongoni mwao ni Mbwana Samatta ambaye kwa mshahara wake peke yake umezua gumzo mtaani,
Sasa taarifa kutoka TFF ambayo ame-amplify Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura unaambiwa Wachezaji watatu kutoka Tanzania ambao ni wachezaji wa mpira wa miguu tayari wameombewa hati ya uhamisho wa Kimataifa[ITC] ili wakacheze katika nchi za Thailand na Ujerumani.
Miongoni mwao ni mchezaji Khamis Mroki Jamal ambaye timu yake ilikua Daraja la Kwanza ya Polisi Dar es Salaam yeye ameombewa ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili akajiunge na Kabinburi ya nchini humo.
Wengine ni Said Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC Turkey ya Zanzibar na Samuel Chuonyo hao wote wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.
Kwa sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika ikiwemo ridhaa ya klabu zao za hapa Tanzania TFF itatoa ITC hizo na jamaa kwenda kujiunga na timu hizo.