Leo June 15, 2018 Tukiwa tunasheherekea Sikukuu ya Eid nikusogezee hii kutoka katika Mgahawa uliopo New York City nchini Marekani ambapo wameanza kupika kuku wa kukaanga huku wakiwa nakshi na dhahabu.
Imeelezwa kuwa watu wengi wamevutiwa na ubunifu huo huku bei za kuku hao zikitajwa kuwa ni kati ya Shilingi laki 1 mpaka Milioni 2 za kitanzania kulingana na idadi ya vipande vya kuku utakavyovinunua.
Aidha imeelezwa kuwa kuku hao wenye dhahabu ni salama kabisa kwa matumizi ya binadamu.
LIVE MAGAZETI: Watapigwa kipigo cha Mbwa koko!, Bajeti yang’ata yapuliza