Leo June 15, 2018 Jumla ya kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 22 zinatarajia kutumika katika kuboresha miundombinu ya barabara mbalimbali zilizopo jijini Arusha kupitia mradi ya Tanzania Strategic Cities Project (TSCP) katika awamu ya pili.
Mradi huo mbali na kuboresha miundombinu ya barabara mbalimbali zilizopo Arusha pia utaboresha mfereji wa maji ya mvua wa Bondeni, ujenzi wa bwawa la kuhifadhia taka ngumu eneo la Dampo Muriet, ujenzi wa vitako vya kubebea vikapu vya kubebea taka ngumu na usanifu wa masuala ya mfumo wa kutolea maji ya mvua.
Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha, Athuman Kihamia alitoa taarifa hiyo katika mkutano uliohitishwa na ofisi ya mkoa wa Arusha ambapo alisema kwamba mradi huo utatekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu na unafadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia(WB).
Kihamia amsema kwamba jiji la Arusha liko katika mradi wa fedha za nyongeza za awamu ya pili kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambapo mradi huo utahusisha maboresho ya barabara za Oljoro kwenda Muriet, barabara ya Njiro, Krokon, Ngarenaro, Sombetini, FFU sanjari na uwanja wa shule ya msingi ya Ngarenaro.
Kihamia amesema Mhandisi Mshauri na msimamizi wa mradi huo ni UWP Consult(T) Ltd na mkandarasi aliyeshinda zabuni ni kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya shilingi, 254 milioni zitatumika kama fidia katika mradi huo.
Hatahivyo,Kihamia amesisitiza kwamba changamoto kuu katika mradi huo ni kuhamisha vifusi katika barabara zinazokarabatiwa huku akisisitiza kuwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo walitumia kiasi cha zaidi ya sh,47 bilioni kujenga barabara zenye urefu wa Kilomita 22.09, ujenzi wa dampo la kisasa eneo la Muriet pamoja na uwekaji wa taa za kuongozea magari kwenye makutano ya barabara za Friends corner ,Col Middleton na Esso.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepongeza hatua zinazofanywa na uongozi wa jiji hilo huku akisema kwamba pamoja na kwamba halmashauri hiyo iko chini ya upinzani lakini serikali imekuwa ikileta fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo bila ubaguzi.
“Pamoja na kwamba jiji la Arusha linaongozwa na wapinzani lakini serikali imekuwa ikileta fedha za kutosha za maendeleo bila ubaguzi hii ndio serikali ya wanyonge” alisema Gambo
LIVE MAGAZETI: Watapigwa kipigo cha Mbwa koko!, Bajeti yang’ata yapuliza