Leo June 18, 2018 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Eng. Isack Kamwelwe amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA kwa sababu ya udanganyifu kuhusu idadi ya visima vya Mpera na Kimbiji Kigamboni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Eng. Kamwelwe amesema hatua hiyo inatokana taarifa iliyoipokea serikali kuhusu udanganyifu huo.
Amesema ubadhirifu huo umefanyika kuhusu idadi ya visima maeneo ya Mpera na Kimbiji Kigamboni.
“Kwa mamlaka niliyonayo nimetengua uteuzi wa Injinia Romanus Mwang’ingo aliyekuwa msimamizi mkuu wa mradi huu kwa niaba ya DAWASA na serikali, ambapo namteua Dk.Sufian Masasi kukaimu nafasi hiyo,” amesema Waziri
Waziri Kamwelwe amesema kwa kuzingatia sheria ya DAWASA ameivunja Bodi ya Wakurugenzi kwa kushindwa kuchukua hatua mapema katika kunusuru mradi.