Michuano ya Kombe la Dunia 2018 inayoendelea nchini Urusi inazidi kupamba moto na baadhi ya majina ya mastaa yameanza kuchukua headlines, mshambuliaji wa Fiorentina anayecheza AC Milan kwa mkopo Nikola Kalinic amezichukua healines leo hii.
Cham cha soka cha nchini Croatia kimethibitisha kuwa Nikola Kalinic ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Croatia na kurudishwa nyumbani, baada ya kugoma kuingia akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Nigeria.
Nikola Kalinic aliambiwa ajiandae ili aingie dakika ya 85 ya mchezo zikiwa zimesalia dakika 5 game kumalizika lakini alisema kuwa hawezi kuingia mgongo unamuuma, kitu ambacho baadae kiligundulika kuwa ni uongo kwani aligoma kuingia kutokana na kupewa dakika 5 za kucheza.
Baada ya hapo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Croatia Zlatko Dalic aliamua kumuamuru Nikola Kalinic kurejea nyumbani Croatia, kwani kitendo alichokifanya ni utovu wa nidhamu na hakikubaliki.
FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018