Leo June 19, 2018 Mhamiaji raia wa Mali Mamoudou Gassama, ambaye alipata umaarufu mkubwa duniani mwezi uliopita kwa kitendo chake cha kupanda juu ya ghorofa mjini Paris, Ufaransa na kumukoa mtoto, amesema amefurahishwa sana kurudi kwao Mali kutembea.
“Nina furaha sana sana kwa sababu kila mtu alikuja uwanja wa ndege na kisha nikamuona baba yangu na watu wote wa familia yangu. Sikuwa nimemuona baba yangu kwa miaka tisa,” amesema Maoudou
Video ya Mamoudou Gassam akimuokoa mtoto ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Alivuka kutoka kwenye baraza moja hadi nyingine kwa muda wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto huyo aliyekuwa amekwama na kumsalimisha.
LIVE MAGAZETI: Kanisa la ajabu Dar, Mbowe yamfika makubwa