Leo June 19, 2018 Naibu Waziri wa kilimo Dr. Mary Mwanjelwa amesema kuwa ni kweli bei ya mbaazi iliporomoka kutoka wastani wa bei ya Shilingi 2750 kwa kilo mwaka 2014/15 hadi Shilingi 700 kwa msimu wa mwaka 2016/17 kwa mikoa mbalimbali hapa nchini.
Ameyasema hayo leo Bungeni Dodoma akijibu swali la Abdallah Chikota lililouliza nini kilichosababisha kuporomoka kwa bei ya mbaazi wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Namnukuu Naibu Waziri Kilimo Dr. Mwanjelwa “Ni kweli bei ya mbaazi iliporomoka, hali hii imesababishwa na ongezeko la uzalishaji wa mbaazi katika nchi za India, China, Brazil, Canada, Msumbijiji, Sudan pamoja na Tanzania,”
“Pamoja na ongezeko hilo la uzalishaji mwezi August 2017 nchi ya India ambayo ndio wanunuzi wa mbaazi za Tanzania ilizuia uingizwaji wa mbaazi kutoka nje ya nchi hiyo kwakuwa walikuwa na uzalishaji mkubwa wa kukidhi mahitaji yao,” -Dr Mwanjelwa
Ameeleza kuwa serikali imekuja na mikakati kadhaa ya kukuza soko la zao hilo kupitia soko la bidhaa (commodity exchange).
Pia alisema kwa maafisa lishe wamekuwa wakitoa mafunzo kwa jamii kuhusiana na umuhimu wa zao hilo kiafya.
Kwa mujbu wa naibu waziri huyo jitihada nyingine ni kuanzishwa kwa kiwanda cha kuchakata mazao aina ya mikunde mkoani Morogoro ambapo kwa siku kitakuwa na uwezo wa tani 200.
LIVE MAGAZETI: Kanisa la ajabu Dar, Mbowe yamfika makubwa