Leo June 19, 2018 Mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa amemtabiria Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa kuchukua jimbo la mtu mkoani Mbeya.
Mchengerwa alikuwa anauliza swali la nyongeza ambapo alisema kuwa kutokana na umahiri wa kujibu maswali wa Naibu waziri huyo atachukua jimbo la mtu huko Mbeya.
Dr. Mwanjelwa ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoa wa Mbeya.
Katika swali lake mbunge huyo alitaka kujua mpango wa serikali wa kuwaandaa Watanzania wanoishi Rufiji kwa kilimo katika bonde la Rufiji.
Akijibu Dr. Mwanjelwa alimshukuru Mbunge huyo kwa kusimamia vizuri kuvunjwa kwa mradi wa kuendeleza bonde la Rufiji (Rubada) ambao haukuwa na faida kwa taifa.
Alisema kuwa kuna hekta 1350 zimetengwa kwa ajili ya mradi wa umeme wa Stigglers Gorge huku hekta laki tatu zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji
Akielezea kuhusu Rubada, alisema kuwa ilikuwa na mapungufu ya ndani na mwaka 2016 bodi iliwafukuza kazi wakurugenzi wawili.
Alidokeza kuwa ilikosa uhalali wa kuendelea kuwepo na mwaka jana serikali ilipeleka muswada bungeni wa kuifuta rasmi.
Ufafanuzi kwa wanaosafirisha Samaki kwaajili ya mboga kutoka Mwanza