Baada ya sakata la Maofisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuingia katika mgahawa wa Bunge na kukagua samaki kwa madai ya kupewa maagizo na Waziri wa wizara hiyo Luhaga Mpina, Spika wa Bunge Job Ndugai leo amesemawataka Wabunge kumsamehe Waziri huyo baada ya kulikosea Bunge.
Ndugai amesema …>>>“Kwa akili ya kawaida watu wananunua samaki kwa kilo na sio kwa futi, sasa hii sheria ya kupima vitoweo hii…! Inabidi hizi sheria tuzisome vizuri, Watanzania wawe wanafunga milango ndio wale samaki?. Kwa kawaida ukakisirishwa sana na jambo unasamehe kwahiyo tusamehe”
Agizo la Dr Tulia kwa Serikali baada ya samaki kukamatwa bungeni